KUPAMBANA NA VITENDO VYA UKATILI SHULENI NCHINI TANZANIA

Mradi huu umefadhiliwa na Wizara ya elimu ya shirikisho la Ujerumani na kuendeshwa na idara ya elimu jumuishi ya chuo kikuu cha Vechta kwa malengo ya kuchangia na kuimarisha ubora wa shule  nchini Tanzania kwa kuzuia vitendo vya ukatili shuleni.Watoto  na vijana nchini Tanzania wanakumbwa na vitendo vya ukatili kwa kiasi kikubwa,uonevu na unyanyasaji wa kijinsia kama utafiti wetu unavyoonesha.

Mradi una sehemu kuu tatu kufikia sasa

Mwanzo ilikuwa ni utafiti wakilishi kwa wanafunzi wa shule za upili za Rulenge wilaya ya Ngara.Dhamira ilikuwa ni kuonesha hali na viwango vya ukatili wanavyokumbana navyo watoto na vijana shuleni nchini Tanzania.

Zaidi ya hayo,katika hatua ya pili na tatu za mradi,hatua za kupambana na vitendo vya ukatili,uonevu,unyanyasji wa kijinsia shuleni.Hivyo,mwongozo umetengenezwa  utakaotumika kwa mazoezi shuleni.

Tunashirikiana na Chuo Kikuu cha SAUT-Mwanza pamoja na Dayosisi ya Kanisa Katoliki ya Rulenge-Ngara(Askofu Severine Niwemuguzi)

Unaweza Kupata habari zaidi juu ya Mambo Tunayoyafanya

MAMBO TUNAYOYAFANYA

Shule Bora nchini Tanzania-Mradi wa Kupambana na vitendo vya Ukatili Shuleni

Usuli

Mkataba wa Umoja wa Mataifa(UN), ulioridhiwa na Tanzania mwaka 1991 unazilazimu nchi wanachama kuwwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili an unyanyasji wa kijinsia .Pia mkataba wa Afrika juu ya Haki na Ustawi wa watoto unazilazimu taasisi za elimu kuweka hatua madhubuti za kwalinda watoto.

Mradi Wetu

Mradi unamalengo ya kuchangia na kuimarisha ubora wa shule  nchini Tanzania kwa kuzuia vitendo vya ukatili shuleni.Watoto  na vijana nchini Tanzania wanakumbwa na vitendo vya ukatili kwa kiasi kikubwa,uonevu na unyanyasaji wa kijinsia.

Mradi una sehemu kuu tatu kufikia sasa.Mwanzo ilikuwa ni utafiti wakilishikwa wanafunzi wa shule za upili (secondary) za Rulenge wilaya ya Ngara.Dhamira ilikuwa ni kuonesha hali na viwango vya ukatili wanavyokumbana navyo watoto na vijana shuleni nchini Tanzania. Zaidi ya hayo,katika hatua ya pili na tatu za mradi,hatua za kupambana na vitendo vya ukatili,uonevu,unyanyasji wa kijinsia shuleni.Hivyo,mwongozo umetengenezwa  utakaotumika kwa mazoezi shuleni.

Maeneo Matatu ya Utekelezaji

Hatua zote zilizopendekezwa zinaingia katika maeneo matatu:

 1. Usimamizi wa Shule
 2. Uhusiano
 3. Mitaala

Usimamizi wa Shule

 • Ofisi inayoratibu shughuli zote ambapo wanafunzi wanaweza kutoa taarifa na kupata msaada
 • Matumizi ya Kamera za Video kwa ajili ya usalama
 • Mfumo wa zawadi na adhabu unaowahusu walimu
 • Mafunzo kwa walimu kwa kutumia mwongozo wa Vechta na kutafsiriwa kwa Kiswahili.

Uhusiano

 • Usuluhishi wa migogoro
 • Vikundi vya wanafunzi shuleni waweze kujumuika muda wa mchana
 • Ushiriki na ushirikishwaji wa wazazi

Mitaala

 • Mafunzo thabiti ya kijamii
 • Mafunzo ya kuimarisha mbinu za ufundishaji kwa walimu
 • Mbinu shirikishi za kujifunzia